KIONGOZI- Ni mtu aliepewa fulsa au nafasi ya kuongoza na kusimamia wengine katika uongozi kuna mambo mengi yanatakiwa kufanyika ili kukabiliana ipasavyo na majukumu yakiutendaji kulingana na nafasi aliyonayo mtu.kiujumla kuna kanuni zakuiongozi ambazo zinaweza kumsaidia mtu/kiongozi kutimiza majukumu yake kikamilifu kanuni hizo ni:
1: KUJITAMBUA NA KUJIKUBALI.
Kiongozi yeyote akishakabidhiwa majukumu cha kwanza lazima ajitambue kwawakati huo kuwa yeye ni nani na kuwa ameshabadilika tayari toka vile alivyokuwa na hivi alivyo, pia lazima ajikubali kuwa watu wamemuona ana kitu cha tofauti ambacho kitafaa katika nafasi aliyopewa hivyo yampasa kutumika kikamilifu.
2:KUTAMBUA WATU UNAO WAONGOZA.
Kama kiongozi unapaswa kuwatambua watu unaowaongoza hii itasaidia kuiandaa akili yako na kutengeneza mazingira mazuri zakuiongozi na mambo yakaenda vizuri.
3:TAMBUA NA FAHAMU MAJUKUMU YAKO.
Kama kiongozi jambo la msingi ni lazima utafute kuyatambua kwa uzuri kabisa majukumu yako kulingana na nafasi iliyopo hii itakusaidia kukabiliana na kupambana na majukumi yako kwa wakati bila kuathiri utendaji kazi wa sehemu husika pia husaidia kugawa na kupanga muda vizuri wa kukabiliana na majukumu yako.
4:TENGENEZA MAZINGIRA YA KUPENDWA,KUHESHIMIWA, NA KUONEKANA UNATHAMANI KATIKA MAZINGIRA ULIYONAYO.
Jamani uongozi sio ubababe uongozi ni hekima na busara ili uongoze vizuri lazima wale unaowaongoza uwatengenezee mazingira ya kukupenda na kukuthamini hii itajenga utii na nidhamu pia itasaidia kazi kufanyika kwa amani sikuzote hakutakuwa na migogoro midogomidogo inayorudisha nyuma maendeleo.
5:ISHI MAISHA YA KIUONGOZI.
Unapokuwa kiongozi lazima maisha yako yawe yakiuongozi yani maisha yamfano maana tayari umeshakuwa kioo mahali ulipo unapaswa,a: jiheshimu
b: thamini utu wa mtu
c:acha upendeleo na ubaguzi
d:usipende kutoa siri za kiofisi
e: kutumia hekima na busara katika mazungumzo usitumie lugha chafu za uzalilishaji zitakushusha thamani.kwahiyo ukiishi maisha haya uongozi kwako utakuwa rahisi sana.
6: JIWEKEE MAZINGIRA YA KUKAKILIANA NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA IDARA YAKO WEWE MWENYEWE.
Kama kiongozi unapaswa kumtengenezea mazingira yakutatua changamoto na watu wako wewe mwenyewe bila kusubiri maamzi ya mtu mwingine hii itasaidia kuondoa muingiliano wa majukumu.
7: JIFUNZE KUKOSOA NA KUOONGEZA.
Kama kiongozi lazima ujifunze kukosoa pale unapoona kitu hakikuenda vizuri ila ukitaka kumkosoa mtu usimkosoe mbele za watu utamfanya adharaulike na kuonekana hawezi kwahiyo muite pembeni na umuelekeze kipi alipaswa afanye, ila ukitaka kumpongeza mtu mpongeze mbele za watu hii husaidia kuamsha hali yautendaji kazi wa wengine kwasababu watu tunapenda kujifunza kwa waliofanikiwa.
8: JIFUNZE KUTUMIA PEMBE TATU AMBUKIZI.
Pembe tatu ambukizi nimsemo wakiuongozi ambao umebeba UPENDO, AMANI NA MSHIKAMANO hii husaidia kuongeza hali ya kiutendaji katika eneo husika kwasababu kwasababu kazi zitafanyika kwa upendo, kutakuwa na amani pia mshikanano baina yaviongozi mliopo na kutengeneza timu yakiutendaji.
9: TUMIA LUGHA RAFIKI ITAKAYOLETA DEMOKRASIA KATIKA MAZINGIRA YAKAZI.
Demokrasia katika uongozi husaidia kupata mawazo mapya yatakayoleta maendeleo sehemu husika pia husaidia kupata mbinu mbadala yakukabiliana na changamoto zilizopo kwenye mazingira husika vilevile husaidia kuongeza hali ya kujifunza na kuleta ushindani wa kiuongozi hivyo kila kiongozi yampasa asimame katika secta yake kikamilifu.
10: PENDA KUJIFUNZA KITU KIPYA KILA SIKU
Hii husaidia kugundua mbinu mpya na bora zaidi zitakazoboresha nafasi uliyonayopia utajifunza vitu ambavyo vitakuwa chachu ya maendeleo mahali husika, hii ni pamoja na kukubali kushaulika.
Penda msemo hii.
NGUVU MOJA SAUTI YA USHINDI
No comments:
Post a Comment