Ufugaji wa kuku unafaida kubwa sana hasa ukizingatia kanuni za ufugaji hasa ufuatiliaji wa tiba na chanjo.leo nawaletea baadhi ya dawa za asili zinazotumika kutibu magonjwa ya kuku. baathi ya dawa hizo ni;
MAJANI YA MWAROBAINI
majani ya mwarobaini hutibu magonjwa yafuatayo;
1;typhodi
2;kideli
3;kuhara
4;mafua na vidonda
chukua majani kipimo cha mikono miwili loweka kwa maji lt 5 loweka ndani ya masaa 10 wape kuku wanywe
SHUBIRI MWITU [ALOVELA]
Alovela hutibu kideli,kuhara,ndui
jinsiya kutumia chukua majani 3 hadi 5 loweka kwa muda wa masaa 10 hadi 12 kisha wape wanywe fanya ivi kwa muda wa siku 5
MBALIKA '[NYONYO]
Nyonyo hutibu uvimbe namna ya kutumia chukua majani yaweke kwenye jivu la moto kisha kanda sehemu iliyo na uvimbe
MLONGE \MLONJE
Chukua majani mikono miwili pondaponda kisha loweka kwenye maji lt 10 kwa muda wa masaa 12 hadi 16
NDULELE,[NDUNGULUSI,MAKONDA,NDULA]
ndulele hutibu minyoo na vidonda jinsi ya kutumia paka sehemu ya vidonda pia unaweza ikaloweka na wakanywa kwaajili ya kutibu minyoo
MAJANI YA MPAPAI
majani ya mpapai pia hutibu magonjwa ya kuku namna takitumia chukua jani moja lipondeponde kisha weka kwenye maji lt 2 wape kuku wanywe
ushauli unapotumia dawa hizi usisahau pia chanjo kwani dawa za asili hutibu taratibu
No comments:
Post a Comment